Na Richard Mwaikenda- Canre, Bonyokwa.
WATANZANIA wametakiwa kuota ndoto kubwa badala ya ndogo ili kupata mafanikio makubwa katika maisha.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), wakati wa mafunzo ya Kilimo Biashara kwa walimu na wanafunzi wa Chuo cha Kilimo, Mifugo na Maliasili (Canre), Dar es Salaam.
"Ukitaka kufanikiwa Ota ndoto kubwa "Bring Big Dream" , acha kuota ndoto ndogo za kitoto zitakazokuchelewesha kupiga hatua za kimaendeleo," alisema Dk. Kissui ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kiuchumi.
Alisema daima amini kwamba ndoto unayoota itakuletea mafanikio chanya na utakuwa nani mbele ya safari.Pia, Dk. Kissui, aliataka watanzania kuachana na tabia ya kutegemea chanzo kimoja cha mapato, bali wawe na ujuzi mwingi, na kubuni vyanzo vingi vya kuwawezesha kumudu maisha yao ya kila siku.
Alisema moja jambo litakalowatoa kwenye lindi la umasikini ni Kilimo Biashara chenye mtazamo wa kuanza kutafuta masoko ndipo ulime zao kwa kiwango na ubora unaotakiwa na mnunuzi.Dk. Kissui alisema kuwa Mkikita inaendesha kilimo kwa kufuata utaratibu huo wa kuanza na masoko halafu ndo kinafuata kilimo. Hivi sasa Mtandao huo unaendesha kilimo cha Papai Salama, Muhogo, Mchaichai na Pilipili kichaa mazao ambayo yote yamepata masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mkikita, Dk. Kissui S.Kissui (katikati), akizungumza katika semina ya mafunzo ya kilimo biashara katika Chuo cha Kilimo cha Canre, Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...