Na Zaynab Nyamka
KLABU ya Singida United imemsimamisha kwa muda usiojulikana mshambuliaji wake raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kambale Salita Gentil kwa utovu wa nidhamu.
Taarifa ya Singida United iliyotolewa leo, kwa vyombo vya habari imesema kwa utovu nidhamu alioufanya Kambale jana kwenye mchezo wa hatua ya 32 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) anasimamishwa mara moja.
Kambale alimpiga ngumi mchezaji wa Green Warriors kipindi cha kwanza na kutolewa kwa kadi nyekundu, hivyo kuiachia mzigo timu wa kucheza pungufu katika sehemu kubwa ya mchezo.Hata hivyo, Singida United ilishinda kwa penalti 4-3 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 na kusonga mbele hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...