Hapa nchini, tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka kila mwaka. Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa, kila mwaka wagonjwa wapya wapatao 50,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali Tanzania. 

Na kati ya hao ni *wagonjwa 13,000 tu, sawa na 26% ndio wanaofanikiwa kufika katika Hospitali zetu kuweza kupata matibabu*. 

Aidha, *wagonjwa walio wengi (takribani asilimia 70) hufika Hospitalini kwa ajili ya matibabu wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa (hatua ya 3 na ya 4)*, hali ambayo hupunguza uwezekano wa wagonjwa kuweza kupona maradhi hayo.

Takwimu za mwaka 2016/2017 kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha kwamba Saratani zinaoongoza nchini ni: 
1. Saratani ya Kizazi ​(32.8%)
2. Matiti ​(12.9%)
3. Ngozi (Kaposis Sarcoma)  ​(11.7%)
4. Kichwa na Shingo ​(7.6%)
5. Matezi ​(5.5%)
6. Damu ​(4.3%)
7. Kibofu cha Mkojo ​(3.2%)
8. Ngozi (Skin)  ​(2.8%)
9. Macho ​(2.4%)
10. Tezi Dume ​(2.3%)

Katika kuadhimisha Siku ya Saratani Duniani *ninatoa wito na kuhimiza kila mmoja wetu kupima ugonjwa wa Saratani. *Saratani inatibika endapo itagunduliwa mapema*. 

Serikali ya Awamu ya 5 inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli itaendelea na jitihada za kuongeza uelewa  wa wananchi juu ya vyanzo mbalimbali vinavyosababisha saratani ili kila mmoja wetu aweze kujikinga. Vyanzo hivi ni pamoja na *Mtindo wa kimaisha (Life Style) kama vile Uvutaji wa sigara, ulaji wa vyakula usiofaa (kula vyakula vyenye mafuta mengi, kutokula matunda na mboga mboga za kutosha), matumizi ya pombe kupita kiasi, matumizi ya dawa za kulevya na kutofanya mazoezi*.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...