![]() |
Marehemu Prof. Hubert Clemence Mwombeki Kairuki na mkewe Mama Kushubila Kairuki; mwanzilishi mwenza wa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN) |
Utangulizi:
Hospital ya Kairuki (KH), Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN) na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kwa pamoja vitashiriki katika maadhimisho ya 19 ya kumbukizi ya Marehemu Prof. Hubert Clemence Mwombeki Kairuki, muasisi wa taasisi mama inayosimamia taasisi hizo yaani Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN).
Kumbukizi hiyo itafanyika kwa juma moja kuanzia tarehe 1 Februari 2018 na kufika kilele chake tarehe 6 Februari 2018, kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama ifuatavyo:
* Kuweka jiwe la Msingi kwenye kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida Bunju.
*Kuanzisha kliniki ya mama, baba na mtoto.
*Kutoa huduma za afya bila malipo kwa wananchi.
*Uchangiaji Damu/Blood Donation.
*Mhadhara wa Tisa wa Kitaaluma wa kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki.
*Mashindano ya kitaaluma baina ya wanafunzi wa HKMU na KSN.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...