Bi.
Sidonia Ntibashigwa ambaye pia anafahamika kama Mama Sophia mkazi wa
Machimbo ya Zamani, Sala Sala Mbuyuni amemshukuru Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia
kiti cha magurudumu (wheel chair).Mama Sophia ambaye alipata ya ajali ya kugongwa na roli tarehe 28 Mei, 2016 Mbuyuni, Salasala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa kumkabidhi kiti hicho Msaidizi wa Makamu wa Rais Siasa Ndugu
Nehemia Mandia alisema “Mheshimiwa Makamu wa Rais aliguswa na suala lako
ambalo liliandikwa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii
kuhusiana na ajali uliyoipata na ulemavu ambao umekupata kutokana na
ajali kutokana na kitendo hicho ameona akusaidie kiti cha magurudumu kwa
ajili ya wewe kufanya shughuli ndogo ndogo unazoweza kufanya”.
Kwa
upande wake Mama Sophia alishukuru sana kwa msaada huo wa Kiti na
kumuomba Makamu wa Rais aendelee na moyo huo huo wa kusaidia wananchi
wake .Alisema kwa sasa bado anaendelea na matibabu kwa sababu mguu wake mmoja bado haujawa na nguvu hivyo hawezi kusimama.
Mama huyo mwenye watoto sita na wajukuu wanne alisema pia bado anahitaji msaada ili aweze kupata matibabu zaidi.
Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Nehemia Mandia (kulia)akizungumza na Bi. Sidonia Ntibashigwa mkazi wa Machimbo ya Zamani Salasala kabla ya kumkabidhi Kiti cha Magurudumu kilichotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Bi. Sidonia Ntibashigwa mkazi wa Livingstone , Machimbo ya Zamani akikabidhiwa kiti cha magurudumu alichosaidiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...