Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wamehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kila mmoja baada ya kukutwa na hatia kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Hukumu hiyo imetolewa leo Feb. 26, 2018 na hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Maiko Mteite baada ya kuridhika ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.
Pia mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha miezi sita katibu wa CHADEMA  kanda ya nyanda za juu kusini Emmanuel Masonga kwa kosa hilo.
Washtakiwa hao wanatajwa kutenda kosa la kutoa maneno ya kumfedhehesha rais Disemba 31, 2017 katika viwanja vya Luanda Nzovwe wakati wakizungumza na wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...