Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Msanii
wa filamu nchini Bibi. Wastara Issa ameendelea kumshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuonyesha
moyo wa kuguswa na tatizo linalomsumbua na kuweza kumpatia kiwango cha
shilingi milioni 15 kwa ajili ya matibabu ya mguu pamoja na mgongo.
Bibi.
Wastara ametoa shukrani hizo jana Jijini Dar es Salaam alipokua
akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa awali ilikua aondoke
nchini tarehe 28 mwezi januari mwaka huu kwenda mjini Mumbai kwa ajili
ya matibabu lakini kutokana na baadhi ya mipango kutokaa vizuri safari
hiyo ilisogezwa hadi jumapili tarehe 4 Februari 2018 ambapo anatarajia
kuondoka mida ya jioni na kufika Mumbai mapema alfajiri siku ya jumatatu
ambapo ataanza matibabu siku hiyo hiyo.
Bibi. Wastara amesema
kuwa katika safari hiyo ataongozana na nesi mmoja kutoka hospitali ya
TMJ pamoja na mtu mmoja kutoka katika familia yake ambapo matibabu yake
yatafanyika katika hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai na kutarajia
matibabu hayo kuchukua takribani wiki tatu na zaidi.
Aidha
msanii Wastara Issa ameishukuru wizara inayosimamia tansia ya filamu kwa
kumfariji katika kipindi hiki kigumu anachopitia huku akimshukuru
Waziri mwenye dhamana na tasnia ya filamu nchini, Bodi ya Filamu
Tanzania, Baraza la Sanaa la Taifa pamoja na watanzania wote kwa
kuonyesha upendo wa dhati kwake.
“Asanteni sana watanzania
mmeonyesha moyo wa dhati kwangu kwa muda mrefu sasa, mmekua pamoja nami
tangu kipindi cha matibabu ya Saduki hadi sasa, uzito wa neno asante
kutoka kwangu leo hauwezi kulipa fadhila kwa dua na michango yenu
kwangu, mwenyezi mungu aendelee kuifanya nchi yetu kuwa na amani na
upendo” amesema msanii Wastara Issa.

Msanii wa Filamu nchini Bibi. Wastara Issa (wapili kulia waliokaa chini) akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kuhusu maandalizi ya safari yake ya matibabu kuelekea Mjini Mumbai walipofanya naye mazungumza jana Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia waliokaa ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...