Kaimu Balozi wa Kuwait nchini, Mohamed Al-Amiri akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuikabidhi Shule ya Msingi ya Jeshi la uokovu vifaa vya walemavu wa viungo na ngozi pembeni yake mwasisi wa Jumuiya ya Albinism Awareness Foundation Suleiman Magoma, Mwalimu wa shule Bi. Flourina Milinga na Afisa elimu taaluma Mkoa Bw. Fortunatus Kagoro
Mwasisi wa Jumuiya ya Albinism Awareness Foundation, Suleiman Magoma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea vifaa vya walemavu wa viungo na ngozi vyenye thamani ya shilingi milioni 30 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya nchi ya Kuwait,pembeni yake aliyevaa kanzu ni Kaimu Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Mohamed Al-Amiri
Kaimu Balozi wa Kuwait nchini, Mohamed Al-Amiri awakabidhi wanafunzi walemavu wa Shule ya Msingi ya Wokovu viti vya matairi,pembeni yake mwasisi wa Albinism Awareness Foundation Suleiman Magoma na Mkurugenzi qa shule Thomas Sinana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...