MTANDAO wa Elimu Tanzania (TenMeT) na taasisi ya Equality Now imekubaliana kufanyakazi kwa pamoja kuhakikisha inapaza sauti za watoto juu ya changamoto mbalimbali za ukatili zinazowakabili hasa watoto wa kike.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika maonesho ya sauti za watoto juu ya changamoto anuai za ukatili zinazowakabili watoto, yalioshirikisha wanachama wa TenMet, Meneja Kampeni wa Equality Now, Bi. Florence Machio alisema matatizo yanayowakumba watoto katika nchi nyingi za afrika yanafanana hivyo kuna kila sababu ya kushirikiana kuyakabili.

Alisema vitendo vya unyanyasaji wa watoto vimekuwa vikiwakatili watoto ndoto zao na kurudisha nyuma Bara la Afrika kielimu, kwani wengi wamejikuta wanakatishwa masomo kutokana na ukatili wanaofanyiwa kama vile kutiwa mimba utotoni, kuozeshwa, vitendo vya ukeketaji na ubakaji dhidi yao.

"Matatizo yanayowakabili watoto nchini Tanzania hayana tofauti na yanayowakabili watoto katika mataifa mengine ya Afrika...hivyo tunapohimiza mabadiliko ya sera na sheria zisizowalinda watoto tuungane kwa pamoja bila kujali unatoka taifa gani," alisisitiza Bi. Machio.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao (kulia) akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya sauti za watoto juu ya changamoto anuai za ukatili zinazowakabili watoto, maonesho hayo yameandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT) kwa kushirikiana na taasisi ya Equality Now.
Meneja Kampeni wa Taasisi ya Equality Now, Bi. Florence Mashio akizungumza kuhusu unyanyasaji wa watoto hasa kwa mtoto wa kike pamoja na namna ya kuupinga ukatili huo wakati wa maonesho ya  ya sauti za watoto juu ya changamoto anuai za ukatilizinazowakabili watoto lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Programu wa TenMet, Bi. Alistidia Kamugisha (kulia) akichangia mada kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wadau kutoka taasisi Binafsi na serikali wakiwa kwenye mkutano uliowakutanisha ili kuangalia namna ya kusaidia mtoto wa kike wakati wa maonesho ya sauti za watoto.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...