‘Kwa
 sasa mama yangu anatumia simu ya kawaida ambayo haituwezeshi 
kuwasiliana kikamilifu kwa njia ya mtandao. Kwa mfano siwezi kumtumia 
picha za wajukuu wake. Ndio maana  nitampa zawadi ya simu hii mpya 
niliyoshinda kutoka Tigo leo ili iturahisishie mawasiliano yetu na 
kumfanya awe sehemu ya ulimwengu wa kisasa wa mawasiliano.’ Haya ni 
maneno ya Margareth Martin Hiza, mfanyabiashara na mkaazi wa Ubungo 
jijini Dar es Salaam ambaye aliibuka moja wa washindi wa simu mpya za 
kisasa senye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 4G katika promosheni ya Nyaka 
Nyaka Bonus inayoendeshwa na Tigo Tanzania. 
Wateja
 wa Tigo Tanzania wanazidi kupata faida lukuki ikiwemo bonasi za hadi GB
 1 bure kwa matumizi yao ya intaneti pamoja na fursa ya kushinda 
mojawapo ya simu janja 900 ambazo bado zinashindaniwa katika Nyaka Nyaka
 Bonus, promosheni murwa inayowazawadia wateja wa Tigo wanaounua vifushi
 vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwaya 
*147*00#. 
Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea  Nyaka Nyaka Bonus, Rajabu Saidi Yote (kulia), ambaye ni mkaazi wa Tandika Dar es Salaam,  akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Jumla ya washindi 156 wamejinyakulia simu katika promosheni hiyo. 
Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea  Nyaka Nyaka Bonus, Tinna Sharon Masatu (kulia), ambaye ni mkaazi wa Mbezi Beach akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Zaidi ya simu 900 bado zinashindaniwa katika promosheni hiyo. 
Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea  Nyaka Nyaka Bonus, Margareth Martin Hiza (kulia), ambaye ni mkaazi wa Ubungo, Dar es Salaam akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Jumla ya washindi 156 wamejinyakulia simu katika promosheni hiyo. 
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


 
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...