Kumekuwepo
na uvumi unaoenezwa kupitia baadhi ya Mitandao ya Kijamii kuwa Idara ya Uhamiaji
imetangaza nafasi za ajira kwa nafasi za Mkaguzi Msaidizi, Koplo na Konstebo. Kufuatia
kuwepo kwa uvumi huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi kuwa:
1. Idara haijatangaza nafasi zozote za ajira
katika kipindi cha hivi karibuni, hivyo tunawaomba wananchi wasirubuniwe au
kushawishiwa na mtu yeyote kutoa kitu chochote ili waweze kusaidiwa kupata kazi
Idara ya Uhamiaji kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na pia hakuna mtu
anayeruhusiwa kulipa fedha ili apate ajira katika Idara ya Uhamiaji.
2. Taarifa za kutangazwa nafasi za kazi zilizotolewa
kupitia Mitandao hiyo ya kijamii hazina ukweli wowote, bali ni uzushi
uliofanywa na watu au kikundi cha watu kwa malengo wanayoyajua wao.
3. Idara ya Uhamiaji,
kama Taasisi ya Serikali inao utaratibu maalum wa kutangaza nafasi za ajira kwa
uwazi kupitia Magazeti, Televisheni na Tovuti yake ambayo ni ‘www.immigration.go.tz’
4. Idara inatoa onyo kwa
mtu au watu wanaojihusisha na utoaji wa taarifa za upotoshaji kupitia mitandao ya
kijamii, kuhusu huduma za uhamiaji ikiwa ni pamoja na suala la nafasi za ajira.
Aidha, Idara haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakao bainika
kujihusisha na vitendo hivyo.
Imetolewa na;
KITENGO CHA UHUSIANO,
IDARA
YA UHAMIAJI
MAKAO
MAKUU, DAR ES SALAAM.
01 FEBRUARI, 2018
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...