Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga.

MBUNGE wa viti maalum Mkoani Pwani,Zainab Vullu amekabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji pamoja na malumalu vipande 500 ,vilivyogharimu sh .milioni 1.6,katika halmashauri ya Mkuranga.

Kati ya vifaa hivyo mifuko 50 ya saruji ni mchango katika ujenzi wa nyumba ya mganga zahanati ya Kijiji cha Koma na mifuko mingine 20 ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kisiju Pwani.

Vullu alielekeza ,Malumalu (tiles)zipelekwe shule ya msingi Kisiju Pwani,katika ujenzi wa vyoo lakini aliomba kipaombele kipewe kwenye vyoo vya wanafunzi wa kike ili kujihifadhi wakati wakiwa katika hedhi .Aidha alisema anahamasisha ujenzi wa nyumba ya mganga na aliwataka wadau wengine waunge mkono jitihada za serikali ,halmashauri ,mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega aliyechangia mifuko 100 ya saruji .

Hata hivyo,Vullu alisema kilichomgusa kuchangia pia ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi inaelekeza kusimamia maisha na maslahi ya mtanzania .
“Kijiji cha Koma hakina zahanati ,kutokana na suala hilo niliona nguvu za Mbunge ,halmashauri na ndipo Jan 1 ,nikwenda kuona hali ilivyo ,nimeona nitoe fedha za mfukoni mwangu nichangie mifuko ya saruji ujenzi wa nyumba ya mganga .” 
KAIMU mkurugenzi halmashauri ya Mkuranga, Mkoani Pwani,ambae pia ni afisa maendeleo ya jamii,Safina Msemo akimshukuru mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani, Zainab Vullu (kushoto aliyesimama)kwa kuchangia baadhi ya mifuko ya saruji kati ya mifuko 70 na malumalu vipande 500 vilivyogharimu zaidi ya mil.1.6
MBUNGE wa viti maalum Mkoani Pwani, Zainab Vullu, akimkabidhi kaimu mkurugenzi halmashauri ya Mkuranga, Mkoani Pwani,ambae pia ni afisa maendeleo ya jamii,Safina Msemo (mwenye gauni la kitenge) baadhi ya mifuko ya saruji kati ya mifuko 70 na malumalu vipande 500 alivyochangia ambapo vimegharimu zaidi ya mil.1.6.Picha na Mwamvua Mwinyi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...