Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

JESHI la polisi mkoani Pwani, limetoa siku saba kwa madereva pikipiki (bodaboda) ambao walitelekeza pikipiki zao katika vituo mbalimbali vya polisi, kwenda kuzichukua baada ya kusamehewa na jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoani humo, (ASP) Jonathan Shanna ,alisema jeshi hilo liliwahi kuendesha zoezi la ukamataji wa pikipiki kwa makosa mbalimbali ambapo baadhi ya madereva walizitelekeza pikipiki hizo hadi sasa.

Hata hivyo alisema ,pikipiki zilizohusika kubeba bangi ,madawa ya kulevya na kutumika kufanya uhalifu hazitatolewa .Alisema wamejiwekea mikakati ya kukabiliana na ajali mwaka huu,kwa kutoa mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa waendesha pikipiki.

Shanna alieleza, watahakikisha wanasimamia elimu hiyo iweze kutolewa kwa madereva hao kwenye vijiwe vyao mitaani kwa kutumia askari waliopangwa kwa kila kata.Pamoja na hayo, watakuwa wanafanya operesheni za mara kwa mara ili kuwakamata wale madereva bodaboda watakaokuwa hawataki kutii sheria bila shuruti kwa kuwachukulia hatua kali na kuwafikisha mahakamani ili kupunguza ajali na vifo kwa waendesha pikipiki.

Shanna alifafanua,wanatarajia kufanya misako kwa magari aina ya Noah yanayozidisha abiria kupita kiasi na magari yanayobeba wanafunzi ambayo hayana ubora .“Tutawachukulia hatua kali na kuwafikisha mahakamani madereva na wamiliki wa magari hayo,yatakayokiuka sheria za usalama barabarani”alisema Shanna.

Shanna hakusita kutoa ushauri kwa mamlaka nyingine ikiwemo wakala wa barabara TANROADS, TARURA, kuwa waongeze juhudi katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa kuweka alama za barabarani na kuziba mashimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...