Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon upande wa wanaume,  Gefrey Kipchumba kutoka Kenya akimaliza mbio kwa kutumia saa 1:03 kwenye uwanja wa ushirika mjini Moshi.
 Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathoni upande wa wanawake,  Grace Kimanzi kutoka Kenya akimaliza mbio kwa kutumia saa 1:13 kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
 Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kulia na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Simon Karikari wakimkabidhi mfano wa hundi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za Tigo Kili Half Marathon wanaume, Gefrey Kipchumba toka Kenya leo kwenye viwanja vya Chuo cha Ushirika mjini Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akiwa na mzee Joram Mollel maarufu kama BABU, mara baada ya kumaliza mbio za kilomita 21 zijulikanazo kama Tigo Kili Half Marathon leo.
 Babu Joram Mollel katikati akiwa na wafanyakazi wa kampuni ya Tigo, pamoja na Mkurugenzi wao Simon Karikari kwa pamoja na kauli mbiu yao TUMETISHA KAMA BABU.
Mshindi wa upande wa wanawake  mashindano ya kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon toka Kenya Grace Kimanzi (katikati) akiwa na washindi wa pili toka Tanzania Fainuna Abdi na mshindi wa tatu, Pouline Nkehenya toka Kenya, wakinyanyua mfano wa Hundi juu mara baada ya kutangazwa kushinda mbio hizo. Kushoto ni waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...