Na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya Dar
WANANCHI wa Kata ya Pugu, Mtaa wa Mustafa, wamempongeza Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita kwa kuwapelekea maji safi na salama huku wakibainishiwa ameweka historia ya kutatua changamoto hiyo.
Kata hiyo ambayo inadaiwa kuongoza kwa changamoto ya maji kwa kipindi kirefu, imejenga historia leo kupitia kwa Meya Mwita ambaye amepeleka maji na hivyo wananchi hao kuondokana na adha hiyo iliyodumu kwa kipindi kirefu.
Meya Mwita ameahidi pia kuongeza huduma hiyo kwenye maeneo ambayo yanachangamoto ya maji.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mtaa huo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mustafa Bahati Lusizi amemshukuru Meya Mwita kwa juhudi alizozionyesha hadi kufanikisha kuwapatia huduma hiyo kwani kilikuwa ni kilio cha muda mrefu.
Amesema tangu kuingia kwa uongozi wake umekuwa wa mafanikio makubwa na kwamba waliomba kwa kipindi kifupi kupatiwa maji huduma hiyo na hivyo wameweza kutekelezewa kwa wakati walioahidiwa.
Amefafanua kwa sasa wananchi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama, nakuomba kufikishiwa kwa huduma hiyo maeneo mengine yenye changamoto hizo.
“ Kwaniaba ya wananchi wa mtaa huu, tunakupongeza Meya umefanya kazi kubwa, eneo hili linachangamoto ya maji, lakini kwa sasa itakuwa historia ,kwenye huu utawala wako tutakukumbuka kwa kutuondolea kero hii” amesema Lusizi.
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (mwenyesuti nyeusi) akitoa maelekezo kwa Diwani wa Kata ya Pugu Bonivesture Mphuru na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mustafa Bahati Lusizi leo alipotembelea kukagua mradi wa maji kwenye kata hiyo, ambapo kwa sasa wananchi hao wameanza kupata maji safi na Salama.
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akimtwisha Mwananchi ndoo ya maji leo, wanao shuhudia tukio hilo ni Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Mwenye suti nyeusi) akiwa na madiwani wa halmashauri ya jiji leo walipotembelea kukagua mradi wa ujenzi wa barabara wa kilomita 0.7 kuingia katika Dampo la Pugu Kinyamwezi ambapo inajengwa kwa kiwango cha zege.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...