TAARIFA KWA UMMA
Kama mnavyofahamu Serikali inaendelea na Mchakato wa kuunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii baada ya Sheria kupita Bungeni. Hivi karibuni kumeibuka taarifa ambazo si sahihi kuhusiana na usalama wa michango na mafao ya Wanachama. Taarifa hizi zimepelekea baadhi ya Wanachama na Wastaafu kuwa na wasiwasi kuhusu hatma ya michango na mafao yao.
Mamlaka inapenda kuwaondoa wasiwasi Wanachama na Wastaafu wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuwa mafao na michango yao iko salama. Waajiri wanapaswa kuendelea kupeleka michango ya wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii husika. Vile vile Wanachama na Wastaafu waendelee kufuatilia mafao yao katika Mifuko kama kawaida hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Dar es Salaam
Tovuti: www.ssra.go.tz
05/03/2018
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...