Na Fredy Mgunda -Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve kwa kuinua uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa kata kumi na saba za wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. 

Akingumza wakati wa baraza la UWT wilaya ya Mufindi Salim Asas alisema kuwa amefurahishwa na mkakati mbunge Rose Tweve kwa kufanikiwa kuwafikia wananchi wa kipato cha chini kabisa ambao ndio wanastahili kuinuliwa kiuchumi kuliko wananchi ambao tayari wanauchumi mkubwa.

“Kwa kweli niwe muwazi kuwa nimefurahishwa na hiki kitu ambacho huyu mbunge anakifanya kwa kuwawezesha wananchi ambao ndio serikali ya awamu ya tano inataka kuwafikia na kuwainua kiuchumi” alisema Asas

Asas aliwata wabunge wengine kuiga mfano wa mbunge Tweve kwa kazi anayoifanya ya kuwawezesha akina mama na wananchi wengi kwa kuwa hiyo ndio inakuwa faida kwa taifa.“Naombeni wabunge wangu wote tufanye kazi kama anayoifanya mbunge Rose Tweve kwa kuwafikia wananchi wa chini ambao mara nyingi imekuwa vigumu kuwafikia kutokana na sababu mbalimbali” alisema Asas
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve kwa kuinua uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa kata kumi na saba za wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. 
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi Rose Tweve akiongea mbele ya baraza kwa kuonyesha furaha yake mbele ya mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas baada ya kuambiwa kuwa ataongezewa shilingi milioni kumi na nane kwa ajili ya maendeleo ya akina wanawake wa wilaya ya Mufindi
viongozi mbalimbali na wabunge wa viti maalum walihudhuria baraza hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...