Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

MWILI wa aliyekuwa Mbunge  wa  Kigoma  Mjini, Mbunge  wa  Bunge la  Afrika  Mashariki na Mwenyekiti mstaafu  wa  Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Kigoma Dk.Amani Walid Kaburu ambaye amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili unatarajiwa kusafirishwa kesho.

Taarifa zilizotufikia zinaeleza mwili wa Dk.Kaburu utasafirishwa kwenda mkoani Kigoma kwa ajili ya kuupumzisha kwenye nyumba yake ya milele.

Dk.Kaburu kabla ya kufikwa na umauti alikuwa Hospitali ya Muhimbili ambapo alifikishwa kwa ajili ya matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili(kiharusi).

Kwa sasa msiba upo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati taratibu nyingine zikiendelea kabla ya kuelekea Kigoma.Michuzi Blogu itaendelea kutoa taarifa za msiba huo kadri zinavyotufikia.

HISTORIA FUPI YA DK.KABURU

Dk. Kaburu alizaliwa 23 Mei mwaka 1949 na enzi za uhai wake amefanya shughuli mbalimbali za ujenzi wa nchi na amekuwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kwenye vyama vya siasa nchini.

Enzi za uhai wake Dk. Kaburu amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema na akiwa kwenye nafasi hiyo alifanya kazi kubwa ya kuuimarisha upinzani na hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema).

Ambapo uongozi wake kwenye nafasi hiyo alifanikiwa kushawishi wananchi wengi wa Mkoa wa Kigoma kujiunga Chadema.Hata hivyo Septemba mwaka 2006 alijiunga na CCM na Oktoba mwaka 2012 akawa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma.

Pia Dk. Kaburu enzi za uhai wake amewahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki kuanzia Juni 5 mwaka 2007 hadi Juni 4 mwaka 2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...