RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Fatma Gharib Bilal ambaye ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.

Mwengine aliyeapishwa ni Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais.

Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said pamoja na Mawaziri.

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Fatma Gharib Bilal  kuwa  Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto katika hafla  iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais katika  hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
 Baadhi ya Mawaziri waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliwaapisha Viongozi hao Fatma Gharib Bilal  kuwa  Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto na Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Balozi Seif Ali Iddi kabla kuwaapisha  Viongozi aliowateuwa hivi karibuni hafla hiyo ya kiapo ilifanyika leo  ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika kiapo cha Viongozi Fatma Gharib Bilal  kuwa  Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto na Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,walioapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo. (Picha na Ikulu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...