Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu Wallace Karia ametuma salamu za pole kwa Chama cha Mpira wa Miguu Cyprus kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Rais wa FA Costakis Koutsokoumnis.

Rais wa TFF Ndugu Karia amesema amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwa kumpoteza mmoja wa viongozi wakongwe wa mpira wa Miguu.

“ Koutsokoumnis alikuwa muhimiri mkubwa kwa soka la Cyprus na amefariki katika wakati ambao Cyprus na mpira kiujumla ulikuwa unamuhitaji,nimesikitishwa na kifo chake na ninatoa pole kwa familia yake,FA ya Cyprus,FIFA na familia ya soka kwa ujumla” Alisema Rais wa TFF Ndugu Karia.

Mpaka mauti yanamkuta Koutsokoumnis alikuwa ndio Rais wa FA ya Cyprus na amekuwa kwenye kamati mbalimbali za FIFA akiwa Makamu Mwenyekiti na alianza kutumikia soka la Cyprus tokea mwaka 1990.

Amewahi kuwa Makamu wa Rais wa FA ya Cyprus kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa FA hiyo mwaka 2001 nafasi aliyoitumikia mpaka mauti yanamkuta.

Koutsokoumnis amefariki Machi 5, 2018 akiwa na miaka 61 baada ya miezi kadhaa ya kupigana kupona ugonjwa wa kansa uliokuwa unamsumbua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...