Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) imeahidi kuimarisha taaluma ya Maendeleo ya Jamii ili iweze kuongeza tija katika jamii.
Hayo yamesemwa mjini Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka wakati wa kikao cha wadau waliokutana kujadili rasimu ya mitaala na kupata maoni yatakayowezesha kuboresha mitaala ya vyuo hivyo.
Bi. Neema amesema kuwa Wizara itafuatilia kwa karibu utoaji mafunzo ya fani ya Maendeleo ya Jamii kwa vyuo vyake inavyovisimamia na pia kushirikiana na Mamlaka nyingine katika kufuatilia utoaji wa mafunzo hayo kwa Vyuo visivyosimamiwa na Wizara.
“Kikao cha wadau cha kupitia mitaala ya vyuo vya maendeleo ya jamii kinajenga uwezo wa Wizara katika kuhakikisha usimamizi wa vyuo hivi unazingatia Kanuni na taratibu za Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jukumu ambalo Wizara imekuwa ikilitekeleza kila inapohitajika” alisisitiza Bi Neema.
Akizungumza katika mkutano huo Kaimu Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George suala la kuwa na mkutano wa wadau kupitia rasimu ya mitaala ya vyuo vya Maendeleo ya Jamii ni hitaji la muhimu ili kupta maoni ya takayosaidia kkuboresha mada, mahudhui, mbinu, stadi za kufundishia na kujifunzia na maarifa.
Mkurugenzi
Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto anayesimamia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, Neema Ndoboka akieleza
mpango wa Wizara katika kusimamia Sekta ya Maendeleo ya Jamii kupitia
Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati akifungua Kikao cha wadau wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya
Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya
Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George.
Kaimu
Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Dkt. Bakari George
akieleza dhumuni la kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya
Maendeleo ya Jamii kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao
hicho cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kujadili Rasimu ya
Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro.
Afisa
Maendeleo ya Jamii, Bw. Abel Palala akiwasilisha mada kuhusu Mtaala wa
mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Stashahada katika kikao cha
kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii katika Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii waliokutana kujadili Mitaala pendekezi ya fani ya
Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa TAFOLI Mjini Morogoro.
Mhadhiri
wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Simon Kilasala akitoa
taarifa ya utafiti wa Soko la ajira kwa wataalam wa Maendeleo ya Jamiki
wakati wa kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya
Jamii kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha
wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wanaokutana kujadili Rasimu ya
Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa TAFOLI Mjini
Morogoro.
Mkufunzi
Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba, Kidubya Kulamiwa akiwasilisha
mada kuhusu Mtaala wa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Astashahada
katika kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya
Jamii katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha siku
moja cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii waliokutana kujadili
Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini
Morogoro.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...