Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameitaka Bodi ya Usajili ya Wakandarasi nchini (CRB) kuwachukulia hatua kali wakandarasi wote walioihujumu Serikali katika miradi ya maji inayotekelezwa nchini.
Naibu Waziri Aweso ametoa tamko hilo mara baada ya kufanya kikao na bodi hiyo na kutaka ufanyike uchunguzi wa kwa miradi yote ambayo utekelezaji wake umegibikwa na utata na wakandarasi wote watakaobainika kutekeleza miradi hiyo wachukuliwe hatua za kisheria.
Amesema hatuwezi kufika popote tukiendelea kuwalea wakandarasi wasio na uwezo ambao wamekuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maji, hatutawaendekeza tena wakandarasi wa aina hii, kwa kuwa wamekuwa chanzo cha kukwamisha juhudi za Serikali katika kuiletea nchi maendelo.
‘‘Naomba mfanye uchunguzi wa kina katika miradi yote ya maji iliyohujumiwa nchini, wizara yangu itawapa ushirikiano wa kutosha ili tuweze kuwabaini wakandarasi waliohusika na ikithibitika kuwa ni kweli wachukuliwe hatua kali na ikibidi wafutiwe usajili kabisa’’, alisema Aweso.
Hata hivyo, amesema wako pamoja na wakandarasi wazawa na watarajie ushirikiano wa dhati kutoka kwa Serikali. Tutawapa kipaumbele wakandarasi wazalendo kwenye miradi ya Serikali na walio waaminifu tutawapa kazi zaidi, tutasimamia na kuhakikisha fedha zao zinalipwa kwa wakati ili watimize majikumu yao kwa ufanisi.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza katika kikao cha pamoja na Wakurugenzi wa Bodi ya Usajili ya Wakandarasi (CRB) katika ofisi za bodi hiyo, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CRB, Joseph Tango na wajumbe wengine wa CRB.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiangalia bomba la maji lililopo kwenye karakana ya Bohari Kuu ya Maji, nyuma yake ni Boharia Mkuu, Crepin Bulamu.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa kwenye karakana ya Bohari Kuu ya Maji iliyopo Boko, jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...