Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kalenda ya FIFA baina ya Taifa Stars na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umemalizika kwa Tanzania kuondoka na ushindi wa goli 2-0 mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo iliyoanza kwa kasi kila upande wakitaka kupata goli la kuongoza ambapo mpaka kufika dakika ya 45 na kwenda mapumziko hakuna timu iliyoona mlango wa mwenzake.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Tanzania wakifanya mabadiliko kwa kumtoa Mohamed Issa 'Banka' na kuingia Ibrahim Ajib kwa ajili ya kwenda kuongeza nguvu katika safu ya kiungo.

Mabadiliko yaliweza kuleta tija ikiwa ni pamoja na kutoka kwa Himid Mao na kuingia Mudathir Yahya kuliweza kuwadhoofisha DR Congo na kupitia dakika ya 75 Mshambuliaji wa kimataifa anayekipiga kwenye kikosi cha Genk nchini Ubelgiji Mbwana Samata anaipatia Tanzania goli la kwanza akimalizia Krosi iliyopigwa na Shiza Kichuya.

DR Congo wakiendeleza kutafuta goli la kusawazisha ila katika dakika ya 88 Shiza Ramadhan Kichuya anaipatia Tanzania goli la pili na la ushindi na kuzidi kupeleka kilio katika timu ya DR Congo.
 Mashabiki wa Taifa Stars wakionesha Uzalendo ndani ya Uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji wa pembeni wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),  Mohamed Issa akiwania mpira na Beki wa Timu ya Taifa ya DR Congo, katika mchezo wao wa kirafiki uliocheshwa kwenye dimba la Taifa, jijini Dar es salaam leo. Taifa Stars imeshinda 2-0.
 mpira wa Juu.
 Beki wa Timu ya Taifa ya DR Congo, Junior Kabananga akimkabili Mshambuliaji wa Taifa Stars, Simon Msuva, katika mchezo wao wa kirafiki uliocheshwa kwenye dimba la Taifa, jijini Dar es salaam leo. Taifa Stars imeshinda 2-0.
Beki kisiki wa Taifa Stars, Kelvin Yondani akimlambisha mchanga Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya DR Congo katika mchezo wao wa kirafiki uliocheshwa kwenye dimba la Taifa, jijini Dar es salaam leo. Taifa Stars imeshinda 2-0.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...