Wilaya
ya Gairo imefanya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8
kupanda miti ili kuashiria uhai kwa wanawake waliokata tamaa. Zoezi hilo
liliongozwa na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel
Mchembe na wanasheria wanawake sita akiwemo Mwanasheria wa Manispaa
Mvomerowaliweza kusikiliza kero za muda mrefu za wanawake.
Masuala
yaliyoangaliwa katika maadhimisho hayo ni migogoro ya ardhi, mirathi,
unyanyasaji kijinsia, ukeketaji na kesi za mimba za utotoni ambapo
zaidi Wanawake zaidi ya 65 waliweza kuhudumiwa. Kauli mbiu katika
maadhimisho hayo wakati wakiendelea katika Uchumi wa Viwanda,
"Tuimarishe usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake vijijini", ambapo
ulipokelewa kwa shangwe na wanawake kijiji cha Kisitwi jambo
lililomvutia Mkurugenzi Bi. Agnes Mkandya na kugawa miche ya korosho
zaidi ya elfu 40, mbegu za pamba na kahawa.
Mhe.
Mchembe alisisitiza wanawake kulima Kilimo cha Kibiashara ili kuinua
kipato na uchumi wao waondokane na utegemezi. Mkuu wa Wilaya huyo
ameziomba Taasisi za kifedha NMB na CRDB kutoa mikopo kwa wanawake
yenye riba nafuu, aidha kabla ya mkopo wanawake wapewe Elimu ya fedha,
masoko, vifungashio, Sheria mbambali na ujasiriamali katika mapana
yake.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akimtambulisha kwa wananchi Mkuu wa dawati la Jinsia Polisi Gairo, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Hope Kimaro wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Wilayani humo.

Mgeni rasmi Mhe. Mchembe akipokea taarifa ya Wanawake Gairo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Gairo, Agnes Mkandya.

Uongozi wote wa Wilaya ya Gairo, upande wa Chama na Serikali ukielekea kwenye kupanda miti kuashiria alama ya uhai mpya kwa wanawake waliokata tamaa.

Viongozi Wanawake wa Wilaya ya Gairo wakiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (wa pili toka kushoto), Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Nyangasi (watatu kushoto) na Agnes Mkandya wakiimba wimbo maalumu kwa ajili ya siku ya Wanawake Duniani. Wilaya ya Gairo inaendeshwa na wanawake kwa asilimia zaidi ya 95 (tisini na tano).

Wanawake wakipima VVU wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Wilayani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...