Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Uongozi wa wa Chama Cha Act Wazalendo wa mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na katibu wao Ernest Kalumuna  wameamua kujitoa katika chama hicho na kujiunga na Chama cha mapinduzi kufuata uzalendo unaonyeshwa na Rais Dr. John Pombe Magufuli.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo aliyekuwa katibu wa Chama hicho mkoa wa Dar es Salaam, Ernest Kalumuna amesema kuwa kutokana na hali mbaya ya Chama chao kilichokuwa kinajisibu kwa misingi ya uzalendo na kushindw akufuata misingi hiyo hasa kwa kiongozi mku wa Chama.

"Tumeshutushwa zaidi na kauli za karibu za kiongozi wa chama chetu ndugu Zitto Kabwe kuhamasisha Viongozi wa Chadema wakae na kufanya maamuzi ambayo anadai sisi tutawaunga mkono huku akimalizia kusema kuwa serikali hii ni rahisi sana kuiangusha  kwa hiyo ni ishara ya juu sana kwa kuona kiongozi wenu wa kisiasa kufirisika"amesema.

Amesema wajumbe wa kamati kuu wakilalamika na wengine wakihama chama kwa sababu hakuna tena kamati  kuu siku hizi lakini kuna kakikundi ka wapambe wake ambao badala ya kujenga wanabomoa.

Alimaliza kwa kusema kuwa wao kama wanasiasa mahiri hawezi kuendelea kuwa kwenye kikundi cha namna hii: "Hivyo kwa pamoja tunatangaza  kujivua  uanachama wa ACT Wazalendo  na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili tufanye Siasa za kweli  za kurudisha nch yetu kwenye misingi ya kuasisiwa kwake", alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...