Wananchi mkoani Kagera wameeleza kero kubwa wanayoipata, ukiwemo usumbufu mkubwa wanapokuwa kwenye shughuli zao nje ya mkoa hasa maeneo ya mpakani kwa kukosa Vitambulisho vya Uraia.
Hayo wameeleza wakiwa kwenye vituo vya Usajili unaoendelea mkoani humo;  ukihusisha Wilaya zote za Mkoa Kagera.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamedai kuwa lengo la kujitokeza kwa wingi ni kutokana na umuhimu wa Vitambulisho hivi; kwani wengi wao hupata shida pindi wanapotoka nje ya mkoa wao ikizingatiwa kuwa mkoa huo upo pembezoni kabisa mwa nchi ya Tanzania.
Wakazi wa kata ya Nshambya Wilaya ya Bukoba ni miongoni mwa wananchi waliojitokeza licha ya changamoto ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Akizungumzia zoezi hilo; Kaimu mtendaji kata ya Nshambya Bi Fatma Christian Majengo, amesema wananchi waliojitokeza ni wengi na kuwataka wananchi wa eneo hilo kutokubali kuuziwa fomu za Vitambulisho vya Taifa, kwani fomu hizo zinatolewa.
Kwasasa zoezi hilo limekuwa linaendeshwa kwa Kata ili kutoa fursa kwa kila mwananchi kupata fursa ya kusajiliwa; hivyo wananchi wametakiwa kuwa makini kufuatilia ratiba ya lini zoezi litafika kwenye Kata zao.

 Wakaazi wa kata ya Nshambia, Bukoba, mkoa wa Kagera wakiwa katika foleni ya kusubiri kupigwa picha wakati wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa licha ya mvua kubwa zilizokuwa zikiendelea kunyesha.
  Afisa uhamiaji Bw. Issa Juma akifanya mahojiano na Bi. Kemilembe Ishengoma wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulishi vya Taifa kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba Mjini.
  Bi. Hadija Abeid, Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akitoa maelekezo kwa wananchi wa kata ya Nshambya waliojitokeza kusajiliwa wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.

 Baadhi ya wakazi wa kata ya Nshambya wakisubiri kukamilisha usajili wa Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi hilo likifanyika katika kituo cha Chuo kikuu Huria kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba.
 Bw. Daniel Michael  Afisa Usajil akimsaidia Bi. Monica Kagasheki kukamilisha zoezi la uchukuaji alama za vidole wakati wa Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...