Airtel Tanzania imetoa gawio linalofikia shilingi bilioni 14.8 hadi sasa kwa wateja wake na mawakala nchi nzima ikiwa ni  sehemu ya faida waliyoipata tangu mwaka 2015.

Hili limebainishwa na Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Airtel wakati akitangaza gawio la robo hii ambalo ni shilingi bilioni 1.8.

“Tangu tuanze kugawa sehemu ya faida yetu kwa wateja mwaka 2015, tumeshatoa jumla ya shilingi bilioni 14.8 na huwa tunagawa kila robo ya mwaka na kuhakikisha wateja na mawakala wanapokea fedha hizi kupitia akaunti zao za Airtel Money na wana uhuru wa kutumia fedha hizi wanavyotaka,” alisema.

Kwa mujibu wa Nchunda, hii ni mara ya sita mfulululizo kwa Airtel Tanzania kugawa sehemu ya faida kwa wateja wake tangu mwaka 2015. “Bwana Pesa hutoa gawio hili kwa wateja wa Airtel Money na mawakala kulingana na salio la mteja kila siku,” aliongeza.

Aliwashukuru wateja wa Airtel kwa kuendelea kutumia Airtel Money na kuifanya iwe huduma yenye tija na maarufu zaidi na kuongeza kuwa hadi sasa wana zaidi ya maduka 100 maalum kwa kutoa huduma ya  Airtel Money ambayo yanafanya huduma hii iwe ya kuaminika zaidi na rahisi kupatikana.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu gawiwo la bilioni 1.8 la robo ya mwaka kwa wateja wa Airtel Money. katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda na Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Marando.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda, akitangaza gawiwo la bilioni 1.8 la robo ya mwaka kwa wateja wa Airtel Money wakati kizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kulia ni Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Marando.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...