Na
Mathias Canal, WK-Dodoma
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama
Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila ametoa ufafanuzi kuhusu
malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd
kama ilivyojadiliwa kwenye Mkutano wao Mkuu tarehe 27/03/2018.
Amebainisha hayo wakati
akizingumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Mjini Dodoma na kusema kuwa Chama
Kikuu cha Ushirika cha Kagera si Kampuni ya kununua kahawa bali ni ushirika wa
wakulima wadogo wadogo wenye lengo la kuunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kuhudumia zao la kahawa na kuliwasilisha sokoni kwa utaratibu
wenye tija endelevu na kisha kugawana mapato baada ya kufanya mauzo.
Alisema bei halisi ya mkulima
kwa upande wa Ushirika inapatikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika ambapo wakulima hulipwa malipo ya mwisho kwa kadri
ya bei ya kuuzia iliyopatikana sokoni na hesabu ya mwisho kuwasilishwa kwenye
mkutano mkuu.
Hivyo kwa vile mchakato
wa mauzo huchukua si chini ya kipindi cha mwezi mmoja tangu mkulima awasilishe
kahawa yake kwenye ushirika hadi malipo ya mwisho kufanyika, basi ili
kumuondolea mkulima adha ya kusubiri malipo yake yote baada ya mauzo wakati
anahitaji kujikimu na kukidhi mahitaji yake muhimu, wakulima wenyewe kwa utashi
wao kupitia Mkutano Mkuu, wanajadili
malipo ya awali atakayotanguliziwa mkulima wakati anasubiri malipo ya mwisho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Mwingine ni Kaimu meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg John kanjagaile. Picha Zote Na Mathias Canal, WK
Waandishi wa habari wakifatilia Mkutano wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Katika Ukumbi wa Ofisi za Wizara ya Kilimo (Kilimo 4).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...