Imeelezwa kuwa Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kwa fursa kubwa za maendeleo ya kiuchumi na biashara kuliko nchi nyingine zote za Afrika Mashariki, na kutolea tuu mfano wa sekta moja ya usafiri na usafirishaji, Tanzania imeelezwa kuwa ni nchi yenye bahati sana, kuzungukwa na nchi 8 ambazo hazina bahari, hivyo fursa tuu za usafirishaji kwa kutumia bandari, reli, maziwa na anga, zikitumiwa vizuri, zinaweza kuipaisha Tanzania kiuchumi na kujiendesha, bila kutegemea sekta nyingine zozote.

Bahati hiyo imeelezwa na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.

John Ulanga, amesema Tanzania imepakana na nchi nyingi ambazo hazina bahari kuliko nchi nyingine yoyote ya Afrika Mashariki, hivyo Tanzania ikichangamkia kutumia fursa hii kibiashara, itakuza uchumia sio tuu wa Tanzania pekee, bali hata wan chi za jirani zetu, na kule kote njia hizi zinakupita, maeneo hayo yana fursa za kustawi kiuchumi.

Ulanga amesema, Tanzania imekana na nchi nane ambazo hazina bahari, nchi hizo ni Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidekrasia ya Kongo, Zambia, Malawi na Msumbiji, na kusema kama tutazizatiti na kusafirisha mizigo yote ya nchi hizi, pato la usafirishaji pekee litakuwa kubwa kuweza kuendesha nchi, hata bila kutegemea sekta nyingine.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt. Diodonne Dukundane, ameishukuru TradeMark kwa ufadhili huo na kueleza fedha hizo zitasaidia sana katika kutimiza majukumu ya CCTTFA ikiwemo uhamasishaji wa matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kuelezea faida za Bandari ya Dar es Salaam ukilinganisha na bandari nyingine.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, akionyesha njia za Ukanda wa Kati, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, kushoto, na a Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt. Diodonne Dukundane wakitia saini mkataba, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, kushoto, na a Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt. Diodonne Dukundane wakibadilishana mkataba, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...