
HUKU
maonyesho ya makazi ya Jebel Sifah yanayoonyeshwa na Kampuni ya Muriya
yenye maskani yake nchini Oman yakiendelea visiwani Zanzibar katika
Hotel ya The Park Hyatt, baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam,
wafanyabiashara wa visiwani hapa wametakiwa kupanua wigo wao wa
kibiashara kwa kununua makazi yao nchini Oman ili wajiwekee vitega
uchumi kwa ajili ya maendeleo yao.
Ushauri
huo umetolewa leo na Meneja Mauzo wa Muriya, Ghizlane El Gouchi, wakati
wa kuelimisha wakazi na wananchi wa Zanzibar juu ya utendaji kazi wao
katika sekta ya ardhi na makazi waliyojikita nchini Oman, huku
wakijivunia maendeleo makubwa kwenye sekta hiyo muhimu dunian kote.
Wadau
wa ardhi na makazi nchini Tanzania, Ali Al Maskary kulia na Aflah Al
Maskary kushoto wakifuatilia jambo na mdau wa ardhi kutoka Oman, Faisal
Said Rashid Alzakwani katika maonyesho ya makazi yanayoendeshwa na
kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman kwa ajili ya kununua
makazi nchini humo. Tukio hilo linafanyika leo Aprili 6, katika Hoteli
ya The Park Hyatt, Zanzibar kuanzia saa nne asubuhi hadi saa moja jioni.
Faisal Said Rashid Alzakwani kushoto akipiga picha na aalozi mdogo wa Oman Visiwani Zanzibar, Ahmad Mohamed Al Muzaini.
Alisema
kwamba ni vyema Watanzania wote wakiwamo wafanyabiashara wakaelewa
umuhimu wa kujitanua kibiashara kwa kuangalia uanIshwaji wa biashara nje
ya mipaka yao, huku Kampuni yao ikifungua milango kwa kuwauzia makazi
kwa utaratibu mzuri na rahisi katika maeneo yenye solo kama vile pembeni
mwa bahari ambako wanaweza kuyatumia kama fursa za kiuchumi bila
kusahau hati ya kuishi nchini Oman.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...