*Majina ya wanaume waliotelekeza watoto kuanikwa hadharani

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MKUU wa mkoa wa Dar es salam Paul Makonda leo April 9 amezungumza na akina mama waliotelekezwa na waume zao jijini Dar es Salaam ambapo mamia ya wanawake hao wamejitokeza wakiwa na watoto zao.

Ambapo ameeleza  maumivu na masimango ya peke yao yamekoma sasa ni mguu kwa mguu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Makonda amesema kuwa mchakato huo utafanyika kwa siku tano na wasaidizi wake wa huduma za sheria watahudumia kwa haki.

Ameeleza hawapo kwa  ajili ya kumkomoa mtu ila ni kulinda haki za Mama na mtoto na kama baba wa watoto hao hawatajitokeza hadharani basi majina yao yatatajwa hadharani.Amesema Makonda  ameeleza wakiona sheria haitoshi watapambana hadi Bungeni kubadili sheria ili kila mwanamke wa kitanzania apewe haki zake pamoja na mtoto  na kuwe na usawa.

Amewataka akina  Mama waliozalishwa na wanaume wa kada zote kama walimu, wanasiasa, walio katika mabenki na kokote Tanzania watatafutwa popote ili kulinda haki za watoto na mama zao.Makonda ameeleza  Serikali Rais Magufuli imewapa kazi ya kuwasikiliza wananchi na hivyo hawapaswi kukaa na madukuduku yao, hivyo walete malalamiko yao kwani watoto wanategemewa kwa mustakabali wa taifa la kesho.

Akizungumza na Michuzi blog Lucy Peter wa Tegeta ameeleza kuwa alitelekezwa mara baada ya kupata ujauzito hadi sasa mtoto wake wa kiume ana miaka 5, na amefika kupata msaada kutoka kwa mkuu wa mkoa ili baba wa mtoto huyo aweze kutoa huduma mtoto huyo kwani hadi sasa mama huyo anaishi kwa wazazi wake.Aidha Nasra Mohammed ameeleza amefurahi kwa hatua ya Mkuu wa Mkoa ya kuwasaidia wamama waliotelekezwa, hivyo anaamini kuwa mtoto wake atapata huduma stahiki kutoka kwa baba yake aliyemwachia mtoto akiwa na mwezi mmoja.

Hata hivyo wamama hao wamefurahi na kumshukuru mkuu wa mkoa kwa kuamua kuwasaidia wao na watoto wao hivyo Mungu ambariki sana.Aidha mkuu wa mkoa ameeleza kuwa watahudumia watu 500 kwa siku na maeneo yote nchini hata kama si mkazi wa Dar es salaam kwani ni haki yao na hakuna kuogopau vitisho vya aina yoyote bali waangalie kupata zao za msingi.
Akina Mama wa MKoa wa Dar es salaam waliojitokeza kupata huduma za kisheria wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wakati wa kupata msaada wa kisheria.
  01.Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Paul Makonda  akizungumza na  waliotelekezwa na waume zao juu   kulinda haki za Mama na Mtoto ambapo kama Baba wa watoto   hatajitokeza hadharani basi majina yao yatatajwa hadharani.(Pacha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
 .Mkuu wa Mkoa akizungumza na maofisa mbalimbali wanaotoa huduma na kusisitiza wawasikilize  wakina mama wote hata wale wasio wakazi wa Dar es salaam. .(Pch na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
 Akina Mama wa MKoa wa Dar es salaam waliojitokeza kupata huduma za kisheria wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wakati wa kupata msaada wa kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...