Na Bakari Majeshi, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemuhukumu mrembo na video queen, Agnes Gerald a.k.a Masogange kulipa faini ya Sh.milioni 1.5 au jela miaka tatu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa zakulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
Hukumu hiyo kwa Masogange imsomwa leo mahakamani hapo Kisutu ambapo Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema, upande wa mashtaka kupitia mashahidi watatu waliopelekwa mahakamani hapo,wamethibitisha mashtaka dhidi ya Masogange kuwa alitenda kosa.
Huku utetezi ukiwa na shahidi mmoja. Hakimu Mashauri amesema,
"Upande wa mashtaka pasipo kuacha wamethibitisha mashtaka, hasa kutokana na uthibitisho uliotolewa na Mkemia Mkuu wa Serikali unaonesha mkojo wa mshtakiwa ulikutwa na chembe chembe za dawa za kulevya.
"Hivyo kutokana na kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka na kuzingatia utetezi wa upande wamshtakiwa ambaye alijitetea mwenyewe, namtia hatiani mshtakiwa kwa makosa hayo ya kutumia dawa za kulevya," amesema Hakimu Mashauri wakati anasoma hukumu hiyo
Hata hivyo kabla ya kusomwa kwa hukumu iliyomtia Masogange hatian, upande wa mashtaka uliombamshtakiwa apewe adhabu kali huku ule wa utetezi ukiomba apewe adhabu ndogo.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amesema, katika kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya Heroinmshtakiwa anahuhukumu kulipa faini ya Sh.Mil 1 ama jela miaka 2, ”Na katika shtaka la pili la kutumia dawa zakulevya aina ya Oxazepam, mshtakiwa anahukumiwa kulipa faini ya Sh.500,000 ama jela miezi 12,"amesema.
Nje ya mahakama hukumu hiyo imezua gumzo kubwa hasa kutokana na watanzania wengi hasa wanaofuatilia mambo ya mastaa wa kibongo walikuwa wakiifuatilia kesi hiyo kwa karibu zaidi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...