Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeendesha semina kwa waajiri wa Mkoa wa Temeke katika jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na waajiri takrabani 200 waliopo katika mkoa wa Temeke kwa mgawanyo wa mipaka ya NSSF.
Akifungua Semina hiyo juzi, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bathow Mmuni, aliwaambia waajiri kwamba sheria mpya ya hifadhi ya jamii imeshasainiwa na Rais na sasa zimebakia taratibu za kiuendeshaji.
‘Semina hizo ambazo zimepangwa kuendelea nchi nzima zikiwa na lango la kuwahimiza waajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati ili kuliwezesha Shirika kulipa mafao ya wanachama kwa ufanisi, kuzijua changamoto zinazowakumba waajiri na kujibu hoja nyingi walizokuwa nazo waajiri kuhusu uelekeo mpya baada ya Mifuko ya Hifadhi ya jamii kuunganishwa na kubaki miwili yaani NSSF na PSSSF’, alisema Mmuni.
Naye Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, James Oigo, akiwasilisha mada kwa waajiri hao alisema, Sheria mpya imefafanua kuwa Mfuko mpya wa waajiriwa wa sekta ya Umma (PSSSF) utakuwa unahudumia waajiriwa wote waliopo katika sekta ya umma wakati NSSF itahudumia waajiriwa wote wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke, James Oigo, akisisitiza jambo wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na NSSF. Kulia ni Kaimu Meneja Kiongozi NSSF Mkoa wa Ilala, Christine Kamuzora na Kaimu Meneja Bima ya Afya NSSF, Zakia Mohamed.
Kaimu Meneja Bima ya Afya NSSF, Zakia Mohamed, akizungumza wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na NSSF.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...