*Azungumzia mambo makubwa ambayo aliyafanya kwenye utawala wake ambayo yatakumbukwa
*Azindua rasmi Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation,aahdi Serikali kutoa ushirikiano mkubwa
*Aelezea Kikwete alivyosababisha awe Rais wa Awamu ya Tano, Kikwete azungumzia malengo ya taasisi

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii.
RAIS Dkt. John Magufuli amesema kwa kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye uongozi wake kuna mambo makubwa ya maendeleo katika nchi yetu huku akitanguliza uzalendo mkubwa na kwamba Watanzania wanamkumbuka na wataendelea kukumbuka watake wasitake.

Pia ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake za dhati kwa Rais mstaafu Kikwete kwa kuweka bayana kwamba ndiye hasa  aliyesababisha yeye awe Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano huku, na kuahidi kuwa atahakikisha Serikali yake inashirikana na Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)ambayo ameizindua rasmi leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

"Mzee wangu Kikwete naomba niseme kutoka moyoni wakati wa uongozi wako umefanya mambo makubwa ya kuleta maendeleo kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzanania.
"Kuna miradi mikubwa ya maendeleo ambayo ameifanya na imeacha alama ambayo itatufanya watanzania tumkumbuke.Kwa kazi ambayo umeifanya kwa uzalendo mkubwa ndani ya nchi yetu Watanzania tunakukumbuka na tutaendelea kukumbuka watake wasitake,"amesema Rais Dk.Magufuli.
Ametaja  mifano mingi hai ya mambo ambayo ameyafanya Rais mstaafu Kikwete kwenye Serikali ya Awamu ya nne na baadhi ya miradi hiyo lipo  la ujenzi wa bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam, ujenzi wa miundombinu ya barabara nchi nzima, ujenzi wa miradi ya maji , umeme na kuimarisha sekta muhimu za afya, kilimo na vijana.
"Rais mstaafu Kikwete alilitumikia Taifa la Tanzania kwa uadilifu mkubwa.Tabia ya binadamu wamekuwa na kawaida ya kumsifu mtu baada ya kufa na kusema pengo halitazibika wakati si kweli kwani kama ni nafasi ya uongozi inaweza kujazwa wakati huohuo.Kwa Rais mstaafu na mzee wangu Kikwete naomba nikusifu ukiwa hai tena upo mbele yangu unatabasamu.Umefanya kazi kubwa ya kizalendo kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzania na unastahili sifa na shukrani kutokana na mchango wao wa kuleta maendeleo kwenye nafasi mbalimbali.
"Ulipokuwa Rais wa Tanzania umefanya mambo makubwa zaidi kwa ajili ya nchi yetu. Katika utawala wako umefanikisha ujenzi wa shule za sekondari za kata , ujenzi wa Hospitali ya Mloganzila na miradi mingine mikubwa ambayo umeifanya na sote ni mashahidi kwa yale ambayo umeyafanya,"amesisitiza Rais Dk.Magufuli na kuongeza mbali ya kuwa Rais mzee Kikwete ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Bara la Afrika na nchi za ulaya na Dunia kwa ujumla na kote huko ametoa mchango mkubwa wa kuleta maendeleo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi kabla ya kuzindua rasmi Taasisi hiyo isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi mara baada ya kumaliza kusoma hotuba yake na kuizindua rasmi Taasisi hiyo isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kabla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JMKF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuizindua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JMKF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuizindua. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...