Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), na Serikali ya Tanzania zimetiliana saini rasimu ya mkataba wa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 15.3, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34, kwa ajili ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, lenye ukubwa wa hekta 3,000.

Rasimu hiyo ya Mkataba imesainiwa na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait, Dkt. Abdulrida Bahman na kwa upande wa Tanzania ikisainiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, mjini Dodoma.Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema hatua hiyo imfikiwa baada ya timu ya wataalamu kutoka Kuwait kutembelea eneo la mradi mkoani Kigoma na kuridhishwa na umuhimu wake kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
“Mradi huo una umuhimu mkubwa kwa watanzania kwa kuwa wataweza kuwa na kilimo cha umwagiliaji cha Mpunga na Mbogamboga kwa mwaka mzima badala ya kilimo cha msimu cha kutegemea mvua, na katika siku zijazo Kigoma itakua miongoni mwa mikoa inayozalisha mchele kwa wingi”, alisema Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali ya Tanzania na Kuwait zitatia saini mkataba rasmi wa mkopo huo wenye masharti nafuu ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu ili mradi huo uanze kutekelezwa ili kuongeza kipato cha wananchi na kuwa na uhakika wa chakula.Amesema Nchi ya Kuwait imekuwa ikiisaidia Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ukarabati wa Hospitali ya Mnazi mmoja, Zanzibar kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SERA), Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, wakibadilishana rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma,

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SERA), Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akisaini rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.
Ujumbe wa wataalamu kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), ukiongozwa na Dkt. Abdulrida Bahman (kushoto), wakisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), kabla ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za  Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akiongoza mazungumzo kabla ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo  wa dola milioni 15.3 za Marekani, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34 kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na mmoja wa wajumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, baada ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34.4, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, tukio lililofanyika mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango).



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...