Na Mwandishi Wetu- Dodoma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inategemea kunufaika na mradi maalum kutoka Shirika la ‘International Youth Fellowship’ lenye makazi yake nchini Korea ya Kusini kuhusu utoaji wa mafunzo ya kuiwezesha jamii kuwa na tabia, fikra na mtazamo  chanya ili kuwa na ari na hamasa ya kufikia mabadiliko ya kweli na endelevu katika kujiletea maendeleo ya jamii yenyewe na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika Kikao kati ya Serikali na Shirika hilo Katibu Mkuu Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amesema  kuwa Mradi huu ni muhimu sana katika jamii ya watanzania kwani utasaidia kubadilisha fikra za watanzania katika kukuza ari na raghba ya kujiletea maendeleo wenyewe katika maeneno yao.

Bibi Sihaba ameongeza kuwa elimu hii itasaidia kuimarisha fikra chanya kwa watanzania wote kujitambua na kuona kuwa maendeleo ya kweli na endelevu yanatokana na ufahamu, uelewa na utashi wa wananachi waliojitoa kufanya kazi za maendeleo kwa kushirikiana na Serikali yenyewe ili kutatua changamoto zilizopo na hivyo  kujifikia maendeleo jumuishi kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Aidha, akizungumza wakati akitoa elimu hiyo kwa ujumbe wa Menejimenti ya Idara kuu Maendeleo ya Jamii, Katibu Mkuu wa Shirika la ‘International Youth Fellowship’ Dkt. Hun Mok Lee amesema kuwa mabadiliko ya fikra ni muhimu katika mendeleo ya Taifa lolote na kama Tanzania inataka kuendelea zaidi inabidi ianze kutoa elimu itakayosaidia kuwajenga na kubadili fikra za watoto na vijana kuhusu utashi wao wa kutatua vikwazo na changamoto ili kujiletea maendeleo yao wenyewe.
  Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akizungumza na wadau wa kutoka Shirika la ‘International Youth Fellowship’ kutoka Korea Kusini wakati walipofika katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma kuwasilisha Mpango maalum kuhusu Umuhimu wa Elimu ya Mabadiliko ya Fikra na Mitazamo katika Kujiletea Maendeleo.
 Katibu Mkuu  Shirika la ‘International Youth Fellowship’ kutoka Korea Kusini Dkt. Hun Mok Lee (kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo hapa Tanzania Jeon Hee Young wakitoa mafunzo kwa Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kuhusu uzingatiaji wa Elimu ya Mabadiliko ya Fikra na Mitazamo katika Kujiletea Maendeleo Jumuishi. 
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai akichangia jambo wakati wa kikao kati ya Wizara na wadau wa Maendeleo kutoka Shirika la ‘International Youth Fellowship’ kutoka Korea Kusini katika ukumbi wa Wizara jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga na Menejimenti yake wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa maendeleo wa Shirika la ‘International Youth Fellowship’ kutoka Korea Kusini mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kujadili uzingatiaji wa Elimu ya Mabadiliko ya Fikra na Mitazamo katika kujiletea Maendeleo Jumuishi kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara jijini Dodoma.
 Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...