Na Ropota Wetu,Globu ya jamii

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),imetoa hukumu kwa vituo viwili vya radio vya Times FM na Clouds FM kwa makosa ya ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam imesema kuwa Radio ya Times FM walitangaza mahojiano na mwanamziki Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinum.

Imeelezwa kwenye mahojiano hayo mwanamuziki huyo alitamka maneno yasiyofaa kimaudhui akimshambulia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza.
"Times FM wamepewa onyo na kutakiwa kumuomba radhi Naibu Waziri Shonza na jamii kwa ukiukwaji huo wa maadili ya utangazaji,"imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Kuhusu Radio ya Clouds FM ni kwamba imepewa onyo kwa kutozingatia mizania ya utoaji wa habari uliohusu pande mbili ya mwanamuziki Ibrahim Musa a.k.a Roma mkatoliki na Naibu Waziri Shonza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...