Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kocha Msaidizi wa kikosi cha Njombe Mji Mrange Kabange amesema kuwa bado wana nafasi ya kuendelea kusalia ligi kuu hata baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba hapo jana.
Njombe Mji walishindwa kutamba kwenye uwanja wa Sabasaba baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa wekundu wa Msimbazi Simba magoli yote yakifungwa na John Bocco.
Baada ya kipigo hicho, Njombe Mji wamesalia katika nafasi ya 15 wakiwa na alama 18 nyuma ya Majimaji inayoshika mkia.
Kocha huyo amesema kuwa, bado wana michezo nane ambapo kama watafaniliwa kuondoka na ushindi wanauwezo wa kuendelea kusalia katika ligi kuu msimu ujao.
"Bado tuna nafasi kuendelea kusalia ligi kuu msimu ujao, tuna michezo nane ambapo mipango yetu ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye mechi hizo na tunaamini tunabaki kwani kikosi changu kina uwezo,"amesema Kabange.
"Kikosi changu kina wachezaji wazuri na wanauwezo wa kukupa matokeo, katika mchezo wa jana hatukuwa vizuri ila mechi zilizobaki tutapambana kufa na kupona kupata matokeo mazuri,"
Njombe Mji ilifanikiwa kupanda ligi kuu msimu wa mwaka 2017/2018 na wameonekana kusuasua hususani raundi ya pili lakini walifanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup na kuondolewa na Stand United.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...