Katika kutekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi kwa kushirikiana na Taasisi ya Wafanyabiashara ya Uholanzi (Dutch Council for International Business - DCIB) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zimeandaa Warsha ya Biashara na Uwekezaji iliyofanyika jijini The Hague nchini Uholanzi tarehe 29/03/2018.

Lengo kuu la Warsha hiyo, pamoja na kuendeleza na kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uholanzi, ni kutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania hususan katika Sekta za Viwanda, Ufugaji, Uvuvi, Utalii, Ujenzi, Kilimo na Miundombinu ya Kilimo. 

Aidha, Warsha hiyo iliyohudhuriwa na Wawakilishi wa Makampuni takriban sitini (60) ni mwendelezo na jitihada mbalimbali ambazo Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa kushirikiana na Balozi za Tanzania zilizopo nje ya nchi kuendeleza diplomasia ya uchumi ili kuweza kukuza uchumi wa Tanzania na kufikia malengo ya Serikali kuwa nchi ya uchumi wa kati na uchumi wa viwanda.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi, Irene Kasyanju,  akitoa neno la ukaribisho wakati wa Warsha ya Biashara na Uwekezaji.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Warsha ya Biashara na Uwekezaji Jijini The Hague wakimsikiliza Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Geoffrey I. Mwambe akitoa mada kwa wahusika wa Makampuni mbalimbali kutoka Uholanzi waliohudhuria Warsha hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...