NA TIGANYA VINCENT -RS TABORA
KAMATI ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora na Wadau wa Usafiri wamependekeza uanzishwaji wa matumizi ya vitabu(log book) kwa magari ya mizigo ili kudhibiti madereva kusafiri mwendo mrefu bila kupumzika na hivyo kusababisha ajali kwa magari yao au kugongana uso kwa uso na magari mengine kutokana na uchovu.
Tamko hilo limetolewa jana wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri mara baada ya kikao cha kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu ya kuondoa ajali za barabarani mkoani humo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitabu hivyo vitasaidia kuonyesha muda alitoka , mahali alitoka na kama amesafiri muda mrefu atalazimisha apumzike ili kuepusha ajali.
Alisema malori yamekuwa yakisafiri mwendo mrefu bila hata dereva wake kupumzika jambo ambalo limesababisha magari hayo yapate ajali au wakati mwingine yawe chanzo kinachosabisha ajali katika magari ya abiria.
Mwanri alisema kwa kulitambua hilo wanaona wakati umefika kwa magari ya mizigo nayo kuwa na vitabu(log book ) inayoonyesha muda alianza safari katika kituo chake cha kwanza na muda alipo baada ya kusimamishwa ili kuona kama kweli amezingatia matawaka ya kitaalamu na sharia ya kutokwenda kasi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akifafanua jambo jana wakati wa kikao cha kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu ya kuondoa ajali za barabarani mkoani humo kichofanyika jana Wilayani Igunga na kuhudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora na ile ya Wilaya ya Igunga na wadau mbalimbali wa usafiri. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo na kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (aliye na kofia ya kijani) akiwa kwenye ilipotokea ajali ya Basi la City Boy kugonagana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiliangalia Basi la City Boy lilopata ajali ya kugonagana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku mara baada kuongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na ile ya Wilaya ya Igunga kutembelea eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye kofia ya kijani) na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na ile ya Wilaya ya Igunga wakiliangalia Basi la City Boy lilopata ajali ya kugonagana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwafariji majeruhi wa ajali ya Basi la City Boy iliyogongana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku mara baada kutoka katika ilipotokea ajali wilayani Igunga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...