Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Mhe. Roeland van de Geer wakisaini Hati ya Makabidhiano ya nyumba nne (4) kutoka Umoja wa Ulaya zilizopo katika maeneo tofauti ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo zimekabidhiwa kwa Wizara na EU baada ya kutumiwa na Umoja huo tokea miaka ya 1975. Baada ya makabiadhiano hayo, Wizara ilizikabidhi nyumba hizo kwa Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA). Makabidhiano hayo yalifanyika Wizarani tarehe 11 Aprili, 2018. 
Balozi Mushy kwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi. Elius Mwakalinga wakisaini hati ya makabidhiano kama ishara kwa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuzikabidhi kwa TBA nyumba nne (4) zilizopokelewa na Wizara kutoka EU.
Balozi Mushy na Balozi Roeland van de Geer wakibadilishana hati hiyo baada ya kusaini
Balozi Mushy na Balozi van de Geer wakionesha hati hiyo .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...