Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni
Mh.Hashim Mgandilwa ameondoa hali ya taharuki iliyokuwa imetanda miongoni mwa
wananchi wa Kata ya Kibada waliowekewa alama ya kubomoa majengo yao na wakala wa barabara (TANROADS) mbali na
kununua viwanja hivyo kihalali kutoka wizara ya ardhi.
Akizungumza na wananchi hao
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye ofisi za Kata ya Kibada
Mh.Mgandilwa amesema kuwa ofisi yake na wataalamu hawapo tayari kuona wananchi
wao wanaonewa.
Aliongeza kuwa mgongano huo
umebainika kwenye mradi wa ujenzi wa barabara uliopo kwenye hatua za awali na
ubainishaji wa mipaka wa Tanroads unaolenga kujenga barabara kiwango cha lami
kuanzia Kibada-Somangila hadi Kimbiji.
Mgandilwa alisema kuwa wizara ya
ardhi ilikuwa na mradi wa viwanja ishirini elfu vilivyouzwa kwa wananchi
kihalali ambapo baada ya Tanroads kubainisha mipaka yake ndipo ilipobainika
kuwa wizara ya ardhi iliuza viwanja vyake hadi kwenye hifadhi ya barabara.
"Viwanja hivi vilinunuliwa
wizara ya ardhi ambapo wananchi walikuwa na uhakika wa usalama wa viwanja vyao
kutokana na kununua kwene wizara husika, leo hii kuja kuwawekea alama ya
kubomoa sio haki, mwananchi anakuwa anawajibishwa kwa kosa ambalo si lake
ndiomaana tumekutana hapa ili tuweze kuona namna gani tunaweza kufikia
muafaka" Alisema Mkuu wa Wilaya.
Aliongeza kuwa wao kama Serikali
wameona ni bora kuzungumza na wananchi
kwasababu Serikali haipaswi kukinzana na sheria badala yake inaangalia
mahali ambapo pamekosewa na kurekebisha.
Aidha Mkuu wa Wilaya aliwataka
wananchi wote waliowekea alama za kubomoa majengo yao ndani ya siku 90 kufika
ofisini kwake siku ya jumamosi tarehe 5/5/2018 ambapo kutakuwa na wataalamu
kutoka wizara ya Ardhi na Tanroads ili kuona namna bora ya kufikia muafaka.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa akisistiza kuwa Sheria itafuatwa kuhakikisha wananchi wanapata haki yao.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa na wananchi wa kibada wakisoma ra,mani ili kubaini mipaka .
Diwani wa Kata ya Kibada Mh.Amin Sambo akishiriki kuchimba eneo
linalodaiwa kuwa na jiwe la mpaka kwenye eneo la mkazi wa Kibada wakati
walipokuwa wakitafuta mawe ya Mipaka.
Kamati ya ulinzi na usalama na waanchi wakizulu kwenye moja ya
nyumba iliyowekwa alama ya kubomoa na wakala wa barabara Tanroads ili
kubaini mpaka uliopo.
Mthamini wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Mpoki Daimon akifafanua
taratibu za uthamini na ulipwaji fidia kwa wananchi wa Kata ya Somangila
Mtaa wa Dege.
Baadhi ya wananchi na wataalamu mbalimbali walishirki kwenye mkutano huo wa hadhara Kibada.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...