TAASISI
isiyo ya kiserikali ya Haftrade Iliyopo Handeni Mjini mkoani Tanga
imeamua kujenga madarasa mawili katika wilaya hiyo ili kuungana na
Serikali katika mpango wa elimu bure.
Akizungumza katika ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa mwishoni mwa wiki iliyopita Handeni Mjini mkoani Tanga Mkurugenzi wa Taasisi ya Haftrade Thecla Mingwa amesema ujenzi wa madarasa hayo upo hatua za mwisho na lengo lao ni kuona wanafanzi wanakaa kwenye mazingira mazuri ya kusomea.
Mingwa amesema Hafrade ina wanachama hai 20 mpaka sasa na kufafanua taasisi yao imesajaliwa kwa ajili ya shughuli za kijamii ikiwemo, elimu,mazingira,afya na maji vijijini. " Taasisi yangu ya Hafrade wakati ikiendelea kusimamia ujenzi huo mkakati wake kutafuta wadau kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari ya Kwenjugo, pia kutoa elimu pamoja na kupanda miti ya matunda na mikorosho" amesema Mingwa.
Amesisitiza mikakati yao mingine ni kutoa huduma zao katika maeneo mengi zaidi huku wakidhamiria kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya tano.Aidha amesema mikakati yao mingine ni kuwa na mashamba makubwa kwa ajili ya shughuli za kilimo.uyaendesha kwa kilimo .Alisema Hafrade inashirikiana na Shirika la Save Children katika shughuli zake mbalimbali katika kuleta maendeleo.
"Hafrade inatoa huduma zake Handeni Mjini yenye Kata, 12 ambazo ni Chanika, Kidereko, Konje, Kwamagome,Kwediyamba,Kwenjugo Mangaribi ,Kwenjugo Mashariki,Mabanda,malezi ,mlimani, msasa na vibaoni,"amesema.Mingwa amesema katika utendaji wa shughuli zake Haftrade imegawanyika katika idara nne ambazo ni idara ya elimu, idara ya Afya, idara ya mazingira, na idara ya maji na inaendesha shughuli zake kwa kushirikiana na Serikali kuakikiasha malengo na mikakati iliyopangwa inatumia.
Ametaja baadhi ya kazi ya idara hizo kuwa ni Idara maji kulinda vyanzo vya maji, idara ya mazingira kuandaa maeneo ya shamba kwa ajili ya kilimo cha shamba darasa.cha mihogo na korosho.

Wanachama
wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Haftrade Ikikagua ujenzi wa Vyoo na
madarasa ambayo wanajenga Katika kata ambazo wanaosimamia mradi Wilaya
ya Handeni mjini mkoani Tanga jana Picha na Heri Shaaban
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...