Hakama Kuu Kanda ya Mtwara leo imetoa  zuio la muda ( temporary injuction) linalozuia matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulation) ambazo matumizi yake yalipaswa kuanza rasmi Mei 5, 2018.


Mahakama imetoa zuio hilo baada ya taasisi sita kuwasilisha mahakamani maombi ya kuzia matumizi ya Kanuni hizo April 30, mwaka huu.

Taasisi zilizowasilisha maombi hayo mahakamani ni Legal and Human Rights Cente (LHRC), Tanzania Human Rights Defenders (THRD), Media Council of Tanzania (MCT), Jamii Media, Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) na Tanzania Editors Forum (TEF).

Taasisi hizo katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo (judicial review) zimewashitaki  Waziri wa Habari, Tanzania Communication Authority (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika maombi ya msingi taasisi hizo zinaiomba Mahakama Kuu kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa kigezo kwamba:-

i) Waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake ( Ultra vires)

ii) Zinakiuka kanuni za usawa (natural justice)

iii) Kanuni hizo zinapingana na haki ya kujieleza ( Freedom of exepression) haki ya kusikilizwa( rights to be heard) , na haki ya usiri ( Privacy rights)

Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa tarehe 10 may 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...