Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa kulipwa wa Tanzania anayekipiga GRC Genk ya nchini Ubelgiji Mbwana Ally Samatta amewapongeza wachezaji wa kikosi cha chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' kwa kunyakua ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Challenge Cup.

Michuano hiyo imefanyika nchini Burundi kwa kuzikutanisha timu za Afrika Mashariki na Kati ambapo kikosi hicho kimerudi na taji nchini.Samatta kupitia ukurasa wake wa Twitter Samatta amewapongeza wachezaji hao kwa kushinda michezo yote mpaka kufikia  hatua ya fainali na kuwafunga timu ya Somalia kwenye mchezo wa fainali.

Pia Samatta amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa na mipango endelevu kwa ajili ya vijana hao  wanaojiandaa na fainali za Mataifa Afrika (AFCON) chini ya miaka 17 yanayotarajiwa kufanyika hapa nchini mwakani.

Serengeti Boys waliowasili jana jijini Dar es Salaam wakitokea Burundi kulipokua kunafanyika michuano hiyo ya CECAFA ambapo wamepokelewa na  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe sambamba na Rais wa TFF Wallace Karia.

Kwa sasa vijana hao wamepewa mapumziko kwa muda kabla ya kurejea tena kambini kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na michuano ya AFCON wakiwa chini ya Kocha Ammy Ninje. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...