Na Mwandishi wetu, Dodoma
WAANDISHI wa habari wanapaswa kuandika na kutangaza habari zao kwa weledi na kuzingatia maadili ili kuepuka kuandika habari zinazoipa serikali sababu ya kufungia vyombo vyao.
Kauli hiyo imetolewa mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania Bw. Ndimara Tegambwage wakati akitoa mada ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania kwenye kongamano la maadhimisho ya siku ya Uhuru Wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo nchini Tanzania yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma.
Kila Mei 2-3 kila mwaka ni siku za kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani.
Aidha katika mada yake hiyo Ndimara alisema Serikali barani Afrika zimekuwa zikikosa uvumilivu na kunyima uhuru vyombo vya habari licha ya kuwa uhuru huo unatambuliwa na katiba za mataifa ya Afrika.
Bw. Ndimara amebainisha kuwa, wakati serikali za Africa zikitoa haki ya kusajili vyombo vya habari hususani Radio, Runinga na Magazeti, serikali zinapokosolewa huvifungia vyombo hivyo kwa tuhuma za kukiuka maadili jambo ambalo alidai kuwa si la ukweli.
Mkongwe huyo wa tasnia ya habari nchini Tanzania amebainisha kuwa serikali nyingi barani Afrika zimekosa uvumilivu na kutumia nguvu nyingi kunyamanzisha wanahabari.
Huku akinukuu hotuba ya Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ambaye ameonya kuwepo kwa wananchi wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya aliwataka waandishi wa habari kuwa makini kutokana na sheria mbalimbali zinazowazunguka zinaohitaji weledi wa hali ya juu katika kuhabarisha.
Awali akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania, Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema Tanzania inautambua mchango wa vyombo vya habari katika kurahisisha mawasiliano ya jamii na kuharakisha maendeleo lakini inakwazwa na kuwepo kwa baadhi ya vyombo vya habari na wanahabari ambao huandika habari nyingi za kutungwa na za uongozi.
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
akifungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya
Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du
Toit akitoa salamu za Unesco wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena
jijini Dodoma.
Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC),
Jane Mihanji akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai kufungua
kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo
akizungumzia malengo ya maendeleo endelevu na jukumu la waandishi wa
habari kutumia nafasi zao kutoa taarifa kuhusu malengo hayo kwa jamii
ili yatekelezeke kwa urahisi, katika kongamano la maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena
jijini Dodoma.
Mtaalamu
wa Masuala ya Vyombo vya Habari na Mkufunzi wa kujitegemea, Rose Haji
Mwalimu akiongoza mjadala kuhusu mada: Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya
Habari na Sheria katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana
inatendeka wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mwandishi
wa Habari Nguli, Ndimara Tegambwage na mwezeshaji wa mada inayohusu;
Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari na Sheria katika kuhakikisha haki
inatendeka na kuonekana inatendeka: wakati wa kongamano la maadhimisho
ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli
ya Morena jijini Dodoma.
Wakili
na Mwandishi wa Habari ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, James
Marenga akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Nashera
jijini Dodoma.
Mdau
wa Habari Ernest Sungura akishiriki kuchangia maoni katika mjadala
uliowasilishwa na mwandishi nguli Ndimara Tegambwage (hayupo pichani)
wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege
(kulia) na Mshauri wa Utawala Bora na Haki za Binadamu wa Ubalozi wa
Sweden nchini, Anette Widholm Bolme wakati wa kongamano la maadhimisho
ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli
ya Morena jijini Dodoma.
Pichani
juu na chini Sehemu ya washiriki ambao ni wahariri, waandishi wa
habari, wadau wa tasnia ya habari na wageni waalikwa waliohudhuria
kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini
yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wakiwemo wahariri, wadau
wa habari na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano la maadhimisho
ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli
ya Morena jijini Dodoma
Mgeni
rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa habari na wafanyakazi wa
Umoja wa Mataifa, Ubalozi wa Umoja wa Ulaya pamoja na wamiliki wa vyombo
vya habari vya kijamii waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya
Morena jijini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...