Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

TIMU ya Taifa ya chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes inashuka dimbani  Mei 12 mwaka huu kuvaana na kikosi cha Timu ya Mali utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ngorongoro Heroes walifanikiwa kuwaondoa timu ya vijana ya Congo DR kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoka sare ya 1-1 hapa jijini Dar  es salaam na 0-0 nchini Congo  kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba

Akizungumza kuelekea mtanange huo Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini.(TFF) Clifford Ndimbo amesema mchezo huo utakaoanza majira ya saa 10 alasir utakuwa ni kwa ajili ya kufuzu kwenda katika fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba. 

Ndimbo amesema timu hiyo ambayo tayari ipo kambini kujiandaa na mchezo huo muhimu na tayari benchi la ufundi limeanza mikakati ya kuhakikisha wanatoka na ushindi ili kuweza kuvuka hatua inayofuata.

Viingilio vya michezo hiyo ni Sh.3000 kwa VIP na mzunguko ikiwa ni Sh.1000 Ngorongoro Heroes inatakiwa kuhakikisha wanatoka na ushindi nyumbani ili mchezo wa marudiano usiwe mgumu kwa upande wao.
TIMU ya Taifa ya chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...