Na Heri Shaaban
SHULE ya Kimataifa  Tanganyika iliyopo Upanga wilayani Ilala jijini Dar es Salaam imetoa msaada wa nguo kusaidia wananchi waliokumbwa  na mafuriko.
Msaada  huo ulitolewa na Mwasisi wa Shule hiyo Ally Dewji ulipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ofisini kwake leo. 

Akizungumza mara baada kukabidhi msaada huo Dewji amesema shule yao ya Tanganyika inafundisha watoto wa miaka minne hadi 12,mara baada kutokea mafuriko hayo wanafunzi wa shule hiyo waliguswa. 

"Wanafunzi wa shule yetu wameguswa wameungana na Serikali leo tumekabidhi msaada wetu kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, "amesema Dewji. 

Dewji ametaja  vitu walivyotoa ni vyandarua, viatu na nguo .

Kwa upande wake  Mjema ameshukuru msaada huo uliotolewa na Shule hiyo  .

Sophia Mjema alisema katika wilaya yaIlala nyumba 70 na shule moja zote ziliathirika na mvua za masika. 

"Misaada hii itapelekwa kwa familia zilizopata mafuriko zote  kila mtu itamfikia,"amesema Mjema  

na kutoa mwito wa kuwataka wananchi wa mabondeni kuondoka mvua kubwa zinakuja hivyo wasikae katika maeneo hatarishi kwa usalama wao.

Wakati huohuo Taasisi ya Khoja Shia Ishanashari Kamat imekabidhidhi msaada wa sinki kwa ajili ya vyoo mia,Taulo za kike na Biskuti. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...