Na Woinde Shizza,Arusha


TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya Wanaume ya Men At Work imeendesha mchakato wa kuchangia damu kwa lengo la kutaka itumike kuwasaidia akina kinamama wanaojifungua na kupoteza damu nyingi.Pia damu hiyo itawasaidia majuruhi wanaonusurika na ajali na kufikishwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru mkoani Arusha.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Maxwell  Stanslaus amesema leo mkoani hapa wameamua kuchangia damu  kama mchango wa wanaume kujitoa kwa ajili ya jamii na kuisaidia jamii kwani wanaume ni nguzo ya familia,jamii na taifa kwa ujumla.Stanslaus amewataka wanaume wote nchini 
kuwajibika na kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii .

"Kwa sasa  tumeamua kushirikiana na kitengo cha damu salama kuchangia damu ili kupunguza changamoto ya upungufu wa damu katika benki ya damu,"amesema Stanslaus .Ameongeza taasisi hiyo ina kazi ya kuwahasisha wanaume wanawajibikaji na kushiriki katika nafasi za malezi  familia na jamii ili kujenga familia imara na hatimaye taifa imara.

Kwa upande wake Mwanachama wa Men At Work Rodgers Nelson amesema kuwa anajisikia faraja kuchangia damu  ili kusaidia kuokoa maisha ya kinamama wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.Kwa upande wa Melayeki  amesema kwake ni mara yake ya kwanza kutoa damu, hivyo amewatoa hofu wananchi kutokua waoga wa kuchangia damu.

Mwanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work akichangia damu
 Wanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Rodgers Nelson   wakichangia damu katika viwanja vya Sheikjh Amri Abeid(picha na Woinde Shizza,Arusha )

Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Maxwell Stanslaus  akizungumza na Mkazi wa Arusha katika zoezi la uchangiaji wa damu lililoendeshwa ma taasisi yake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...