Na Chalila Kibuda, Globu Jamii
TIMU ya Ngobanya imeibuka mshindi katika fainali ya May Day
Tornament baada ya kuibamiza Timu ya Lake Cement kwa bao 2-1
katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kimbiji Kigamboni jijini Dar
es Salaam.
Mgeni rasmi katika fainali hiyo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa
Manispaa ya Kigamboni Wangeslaus Lindi ambapo amesema
mpira wa miguu unaibua fursa kwa vijana kuonyesha kipaji na
baadaye kujipatia kipato.Amesema utaratibu unaofanywa na Kiwanda cha Saruji cha Lake Cement ni mzuri katika kujenga uhusiano mzuri kati ya kiwanda na wananchi wanaozunguka kiwanda hicho.
Kwa upande wa Meneja wa Rasilimali Watu, Julieth Domel
amesema wamekuwa na utaratibu wa kufanya mashindano kila
mwaka katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi na maendeleo
mazuri ikiwemo uboreshaji wa ligi hiyo.
Amesema mwakani kutakuwa na maboresho ya ligi hiyo ikiwa na
lengo la kuibua vipaji kwa wakazi wa Kimbiji .Ofisa Uendeshaji na Mkuu wa Kiwanda hicho, Girdhari Jadhao amesema kuwa kama kiwanda ni wajibu kuwa karibu na wananchi wanaozunguka kiwanda hicho .
Kocha wa Timu ya Lake Cement, Azizi Senzey amesema wamekubali
matokeo na watajipanga katika kipindi kingine katika kuchukua
ubingwa.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Wangeslaus Lindi akizungumza katika fainali ya kati ya timu ya Ngobanya na Nyati iliyofanyika katika kiwanja cha Kimbiji, jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Wangeslaus Lindi akikagua timu ambazo zilikuwa katika dimba ya fainali zilizofanyika katika kiwanja cha Kimbiji.
Meneja wa Rasilimali Watu, Julieth Domel akizungumza kuhusiana na ufadhili wa Lake Cement katika mashindano mbalimbali ya kujenga ujirani mwema yaliyofanyika katika Uwanja wa mpira cha Kimbiji ,Jijini Dar es Salaam.
Kocha wa timu ya Nyati, Aziz Senzey akizungumza kuhusiana na kushindwa kuibuka kidedea katika fainali kati ya Ngobanya na Nyati katika mchezo uliochezwa katika uwanja cha Kimbiji jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watazamaji wa mashindano ya fainali kati ya Ngobanya dhidi ya Nyati, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kimbiji , jijini Dar es Salaam.
Mashindano ya kamba katika fainali za mpira wa miguu yaliyofanyika uwanja wa Kimbiji
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...